Marekani imetangaza vizuizi dhidi ya kampuni 4 za Kichina kwa madai kujihusisha na juhudi za utawala wa Beijing za kuboresha Jeshi la Ukombozi wa wananchi nchini China.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imeeleza kuwa vizuizi hivyo ni dhidi ya Shirika la Kimataifa la Uzalishaji la China Semiconductor (SMIC), Shirika la Mafuta la Pwani ya China (CNOOC), Kampuni ya Ushauri ya Uhandisi ya Uchina na Kampuni ya Teknolojia ya Ujenzi ya China.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying, amesema hatua zilizochukuliwa na Marekani dhidi ya kampuni za Kichina ni kitendo cha shinikizo halisi la kisiasa na kubainisha kuwa China itachukua hatua muhimu kulinda haki na maslahi yake.
Uamuzi huo unafanya idadi ya kampuni zilizojumuishwa kwenye orodha ya vikwazo ya Marekani kuongezeka hadi kufikia 35.