Ubalozi wa Marekani nchini Iraq umesema kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeamrisha kuondoka nchini humo kwa wafanyakazi ambao si wa dharura.
Hali hiyo inakuja kufuatia mzozo unaozidi kuongezeka baina ya Marekani na Iran ambapo siku za hivi karibuni malumbano na vitisho kwa pande zote mbili umeongeka.
Katika taarifa ubalozi huo umesema amri hiyo ni kwa ajili ya wafanyakazi ambao si wa dharura katika ubalozi huo wa Baghdad na ubalozi mdogo ulioko mji wa Erbil katika eneo la Iraq linalojiongoza lenyewe la Kurdistan.
Aidha, kulingana na taarifa hiyo utoaji wa kawaida wa huduma ya Visa utasimamishwa kwa muda katika hizo balozi mbili mpaka pale muafaka kati ya nchi hizo utakapopatikana.
Raia hao wa Marekani wametakiwa kuondoka nchini Iraq haraka iwezekanavyo, huku amri hiyo inakuja siku moja baada ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani kusema kuwa vikosi vyake nchini Iraq na nchi jirani ya Syria viko katika tahadhari kubwa kufuatia kitisho cha kuaminika kutoka kwa vikosi vya Iran eneo hilo.