Marekani kupitia Balozi wake kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa ameilaumu Korea ya Kaskazini kwa kulazimisha vita kutokana na kuendelea na majaribio yake ya makombora ya nyuklia ya masafa marefu.
Balozi Nikki Haley ametaka kutangazwe kwa hali ya dharura na Baraza la Umoja wa Mataifa kwaajili ya kuishughulikia Korea Kaskazini kuhusu mpango wake inaoendelea nao wa majaribio ya silaha za nyuklia.
“Marekani haihitaji kupigana vita, na vita si kitu kizuri hata kidogo, lakini uvumilivu ukitushinda hatutasita kuitandika Korea Kaskazini, kwani kwa sasa tunatumia njia ya kidiplomasia kutatua tatizo hili,” amesema Haley.
Aidha, wakati mazungumzo hayo yakiendelea, Korea Kaskazini inajiandaa kuendelea kufanya majaribio yake mengie ya makombora ya masafa marefu kitu ambacho kinapingwa na Marekani.
-
Video: Hukumu ya Kenya yaendelea kutikisa nchini, DCI akiri utata miili ya viroba
-
Marekani yatishia kuitwanga Korea Kaskazini
-
Korea Kaskazini kufanya majairibio zaidi ya makombora
Hata hivyo, kwa upande wake China imezidi kusisitiza wito wake wa kutaka pande zote zirudi katika meza ya mazungumzo ambayo inaona kuwa ni suluhisho la kumaliza mgogoro huo.