Marekani imekubaliana na pendekezo la kushiriki katika mazungumzo yanayoihusisha Iran na nchi nyingine zenye ushawishi mkubwa duniani kwa lengo la kufufua mkataba wa nyuklia.

Iran iliapa kudhibiti mpango wake wa nyuklia kwa masharti ya kuondolewa vikwazo vya kiuchumi chini ya mkataba wa nyuklia wa 2015, lakini Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliiondoa Marekani katika mkataba huo mwaka 2018, hatua iliyoifanya Iran kuvunja ahadi zake.

Chini ya utawala mpya wa Rais Joe Biden, Marekani imeonesha nia ya kujiunga tena na mkataba huo.

Siku ya Alhamisi, Utawala wa Biden umekariri ahadi yake ya kujadiliana na Iran kuhusu mkataba huo, unaofahamika kama Mpango wa pamoja wa kina wa utendaji- (JCPOA).

Utafiti wa TALIRI ulivyolenga kutatua changamoto za wafugaji
Rais Magufuli amlilia Balozi Kijazi, asisitiza maombi