Seneta maarufu nchini Marekani, John McCain, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81 katika chumba chake cha mapumziko.
McCain alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya ubongo, amefariki katika chumba chake cha mapumziko mjini Sedona, Arizona, akiwa na familia yake.
Aidha, mwanasiasa huyo mkongwe aligundulika kuwa na ugonjwa huo hatari mwezi Julai mwaka 2017 ndipo alipoanza matibabu rasmi.
McCain aliwahi kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican mara mbili, na kuteuliwa kama mgombea rasmi mwaka wa 2008 ambapo alipambana na kushindwa na mgombea wa chama cha Demokratic, Barack Obama.
Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa maombi yake anayaelekeza kwa familia ya Seneta McCain ambaye aliwahi kulitumikia bunge la Marekani kwa miongo mitatu na aliwahi kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican mara mbili, na kuteuliwa kama mgombea rasmi mwaka wa 2008 ambapo alipambana na kushindwa na mgombea wa chama cha Demokratic, Barack Obama.
-
Barabara ya chini ya Ardhi ya kusafirisha dawa za kulevya yagundulika
-
Jean Pierre Bemba atupwa nje mchakato wa uchaguzi Congo DRC
-
Papa Francis awasili Ireland kwa masikitiko
.