Rais wa Marekani, Donald Trump ameizungumzia Korea ya Kaskazini baada ya kitendo chake cha hivi karibuni cha kurusha kombora lenye uwezo wa kubeba silaha za kinyuklia kwamba nchi hiyo ni hatari kwa usalama wa dunia.
Trump ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi ya Canada, Justin Trudeau katika ikulu ya Marekani, Trump amesema kwamba ataishughulikia Korea ya kaskazini mpaka pale itakapo acha kfanya hivyo.
Aidha, baraza la usalama la Umoja wa mataifa lina nia ya kufanya mkutano wa dharula muda cha kuijadli korea kaskazini kwa kitendo ilicho kifanya korea.
Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Geng Shuang amesema kwamba Beijing ililipinga jaribio hilo, inagawa Pyongyang ilikuwa inaendelea na mipango yake ya uendelezaji silaha kutokana na mvutano ulioko baina ya Washington na Seoul