Siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuongea kwa simu na Kiongozi wa Taliban, Marekani imewashambulia kwa ndege wapiganaji wa Taliban hapo jana, Machi 04.

Kanali Sonny Leggett amesema mashambulio hayo yalikuwa ya kujihami dhidi ya Wapiganaji wa Taliban waliokuwa wakishambulia Kituo cha Ukaguzi cha Jeshi la Afghanistan huko Nahr-e Saraj, Helmand.

Shambulio hilo limekuja siku chache baada ya Marekani na Taliban kusaini makubaliano ya kusitisha vita vilivyodumu kwa miaka 19 huko Afghanistan.

Hata hivyo, Msemaji waTaliban ameeleza kuwa kundi hilo litaendelea kupigana mpaka hapo makubaliano ya ndani yatakapofikiwa.

Msemaji wa Polisi wa Helmand, Mohammad Zaman Hamdard amesema kwa siku za Jumatatu na Jumanne wameshuhudia mashambulio makubwa ya Taliban ambapo zaidi ya Askari 20 waliuawa.

Waziri mkuu amuwajibisha meneja TANROADS Morogoro
Italia yafunga shule na vyuo kujikinga na Corona, facebook yafunga ofisi