Marekani imeionya Syria dhidi ya matumizi ya silaha zenye kemikali ambazo inatarajia kuzitumia dhidi ya kikundi cha wanamgambo wa Islamic State.
Aidha, taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imemuonya rais wa Syria, Bashar al Assad kuwa endapo atatumia silaha zenye sumu basi Marekani itamchukulia hatua kali zikiwemo kuishambulia nchi hiyo.
Imesema kuwa shambulio lolote litakalofanywa na Syria lenye silaha zenye sumu dhidi ya wanamgambo wa Islamic State litasababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia.
Hata hivyo, Marekani imeongeza kuwa iko Syria kwaajili ya kukabiliana na wanamgambo wa Islamic State lakini imeionya Syria kuwa kama itafanya shambulizi lolote lenye silaha zenye sumu itakiona cha moto.