Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni leo bungeni ametoa ufafanuzi kuhusiana na swali la nyongeza lililoulizwa na Peter Msigwa kuhusiana na tuhuma dhidi ya jeshi la polisi ya kukamatakamata watu na kuweka ndani ziadi ya masaa 24.
Amesema kwamba ni kweli kwamba dhamana ni haki ya kila raia na inataka mtu akae ndani masaa yasiyozidi 24.
Ambapo ameeleza kuwa sheria ya makosa ya jinai imeweka masharti na utaratibu wa dhamana hiyo katika ibara ya kifungu cha 148 ambacho kimeanisha aina ya mokosa yanaweza kumfanya mtu akae ndani zaidi ya masaa 24 katika kituo cha polisi.
-
Serikali yafanya mabadiliko TTCL
-
Ukata walikumba jeshi, lakosa pesa ya chakula na maji
-
Ahadi za mbunge CUF zawakosha wananchi
Amefafanua baadhi ya mambo yaliyoainishwa katika sheria hiyo.
Na kusema kuwa polisi inaweza kuumba kibali kutoka kwa mahakama ikiwa haijakamilisha upepelezi wake na kutaja makosa mambayo hayapaswi kupewa dhamana mfano kuuwa kwa kukusudia, ubakaji, ujambazi, ugaidi au mtu ambaye amekiuka masharti ya dhamana.
Ameongezea kuwa ikiwa polisi ikijiridhisha kumpatia dhamana mtu huyo kunahatarisha maisha yake au jamii inyozunguka, basi mtu huyo anaweza kuwekwa ndani kwa masaa zaidi ya masaa 24.
Lakini ikiwa kuna mtu amekaa polisi zaidi ya masaa 24 kinyume na mambo yalioainishwa katika sheria hiyo ya makosa ya jinai, basi taarifa hiyo tuletewa ili tuchukue hatua.
Aidha serikali ya awamu ya tano jeshi la polisi limejipanga kufanya kazi kwa uweledi na kwa kufuata sheria kwa uadilifu kwani hata malalamiko mengi ya wananchi yamepungua kwa kasi sana.