Mgombea wa ubunge kupitia chama cha CUF, Rajab Juma wakati akijinadi katika kampeni amesema akichaguliwa atapeleka hoja binafsi bungeni kuitaka Serikali itoe angalau mlo mmoja kwa wanafunzi ili watulie shuleni.

Pia ameongezea kuwa ataweka utaratibu maalumu wa kuwasajili wafanyabiashara wadogo ili watambulike na wajiwekee akiba yao na yeye kama mbunge wao atatia mkono wake kidogo.

”Nikichaguliwa nitashinikiza serikali iongeze maslahi ya walimu ili wasifikirie kufanya biashara ndogondogo badala yake wafundishe kikamilifu ”amesema.

Amesema akichaguliwa ataanzisha mfuko maalumu wa bima ya Afya kwa ajili ya wanawake na watoto ili watibiwe kwa gharama nafuu.

Mgombea huyo amesema kwamba akiwa mbunge atabainisha maeneo ambayo watachimba visima kwa ajili ya kuwapatia wananchi maji safi na salama.

Aidha amesema kuwa tatizo liliopo kwenye uchaguzi huo si kumpigia mgombea wa CCM bali kubadilisha mfumo.

Na mtu wa kubadilisha mfumo huo ni Rajab Juma.

 

Nigeria yajenga barabara kupita ndani ya ngome ya Boko Haram
LIVE: Rais Magufuli katika maadhimisho ya wiki ya sheria