Baaada ya kuambulia kipigo cha mabao 1-2 nyumbani kutoka kwa Ruvu Shooting, mashabiki wa Mbeya City wamemjia juu kocha wao, Mubiru Abdallah.
Mbeya City wamekuwa wakisuasua kwenye ligi msimu huu hali inayowafanya kuwa kwenye hatari ya kuingia katika janga la kushuka daraja licha ya kushika nafasi ya kumi.
Wagonga nyundo hao wa Jiji la Mbeya, wamejikusanyia alama 27 katika michezo 25 waliyocheza, bado michezo mitano kumaliza msimu huu.
Wakizungumza jijini Mbeya mashabiki hao wenye hasira kali, wamesema kocha Mubiru ameshindwa kabisa kurejesha makali ya timu hiyo.
“Kocha anazingua sana na mbinu zake zimefeli kabisa maana unaona timu haina uwezo kabisa wa kupambana tofauti na msimu uliyopita,” alisema mmoja wa mashabiki hao.
Mbeya City katika michezo mitano iliyosalia, mitatu itacheza ugenini dhidi ya Namungo FC, Kagera Sugar na Geita Gold, kisha itamalizia miwili nyumbani dhidi na KMC ambao Dimba la Nelson Mandela mkoani Rukwa.