Beki wa Kulia wa Simba SC mwenye uwezo wa kupandisha mashambulizi na kulinda lango la timu hiyo Shomari Salum Kapombe, ameweka wazi kuwa watapambana kufikia malengo ya kutinga Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu 2022/23.

Simba SC tayari imeshacheza michezo minne ya Kundi C, huku Kapombe akiwa sehemu ya Wachezaji walioanza katika kikosi cha kwanza kilichoeza michezo yote, huku akishuhudia timu hiyo ikifungwa mabao manne na wao wakifunga mabao mawili.

Ikumbukwe kuwa, awali timu hizo zilipokutana mjini Conakry nchini Guinea, Simba SC ilipoteza kwa kutunguliwa bao moja, hivyo ina deni la kulipa kisasi katika mchezo ujao.

Kapombe amesema: “Sio kazi rahisi kwenye mashaindano ya kimataifa kupata matokeo mazuri, ambacho tunakifanya ni maandalizi na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.”

“Ninaamini kwa mechi ambazo tunacheza tunazidi kuwa imara, hivyo tutapambana kupata matokeo mazuri, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”

Simba SC itakuwa mwenyeji wa Horoya AC katika mchezo wa Mzunguuko watano wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika siku ya Jumamosi (Machi 18), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC inaelekea mchezo huo ikihitaji alama Tatu tu ili kufikisha Tisa zitazoifanya ifuzu moja kwa moja na kuungana na Raja Casablanca ya Morocco iliyofuzu baada ya kufikisha alama 12.

Kimbuka Freddy: Zaidi ya 100 wafariki hali ya hatari yatangazwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 14, 2023