Mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Senegal dhidi ya Ivory Coast uliochezwa jijini Paris nchini Ufaransa, ulilazimika kusitishwa kabla ya dakika 90, baada ya mashabiki kuvamia sehemu ya kuchezea dakika ya 88.
Tukio hilo lilitokea ikiwa tayari timu hizo za Afrika magharibi zikiwa zimefungana bao moja kwa `moja.
Mwamuzi Tony Chapron aliwaamuru wachezaji kurejea katika vyumba vya kubadilishia, kwa kuhofia hali ya usalama wao ambayo huenda ingeharibiwa na mashabiki waliovamia sehemu ya kuchezea.
Wahusika wa usalama walijitahidi kuwaondoa mashabiki sehemu ya kuchezea, lakini hatua hiyo ilishindikana na kumlazimu mwamui kumaliza mchezo huo.
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane alikua wa kwanza kuipatia Senegal bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati dakika ya 68, lakini Gohi Cyriac aliisawazishia Ivory Coast dakika tatu baadae.