Uongozi wa Simba SC umewatoa hofu Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kuhusu mkataba wa Kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama.
Chama amekua akitajwa sana na baadhi ya Mashabiki na Wanachama akidaiwa huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu, kutokana na Uongozi kuwa kimya katika suala la kumsainisha Mkataba mpya.
Ahmed amesema Chama hataondoka Klabuni hapo kama inavyodhamiwa, kwani bado ana Mkataba na Klabu hiyo na Uongozi unafahamu nini unachokifanya.
“Chama alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu na tayari nusu aliitumijia msimu uliopita na sasa hivi tayari ametumikia nusu nyingine.”
“Kwenye mkataba wa miaka miwili na nusu ametumikia mwaka mmoja pekee bado ana mwaka mmoja na nusu. Wanachama wa Simba wasiwe na wasiwasi, Chama bado yupo sana Simba.”
“Siku hizi watu hawatanii wanafanya kweli, kwa hiyo watu wako muhimu lazima uwafunge kwa mikataba mirefu ili wafanye kazi kwa utulivu.” amesema Ahmed Ally
Wakati huo huo Kikosi cha Simba SC leo Jumatano (Desemba 28) kinarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Mzunguuko wa 19 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’.
Wachezaji wa kikosi cha Simba SC walipewa mapumziko ya kwenda kukutana na Familia zao, walipewa Mapumziko hayo baada ya kikosi hicho kurejea jana Jumanne (Desemba 27) jijini Dar es Salaam kikitokea mkoani Mwanza ambako kilicheza mchezo wa Ligi Kuu juzi Jumatatu (Desemba 26) dhidi ya KMC FC mchezo ambao walishinda 3-1.
Simba SC itacheza dhidi ya Tanzania Prisons Jumapili (Desemba 31) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.