Takriban watu 28 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti, likiwemo lile lililotokea katika eneo la Cascades, magharibi mwa nchi ya Burkina Faso ambalo limegharimu maisha ya watu 15. na lile la Falangoutou la eneo la Sahel ambalo limeua watu 13, wakiwemo askari 10.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la nchi hiyo, imeeleza kuwa, “limetokea shambulio la kigaidi dhidi ya askari na wanajeshi wa kujitolea kwa ulinzi wa nchi, wasaidizi wa jeshi la Burkina Faso, waliokuwa wakipiga kambi huko Falagountou, eneo ambalo liko mbali na mpaka na Niger.”
Aidha, taarifa hiyo imedai wahusika wa shambulio hilo ni kundi lenye silaha ambalo lilijitolea kushambulia raia baada ya kushindwa wiki chache zilizopita na vikosi vilivyojitolea kurejesha maeneo yanayodhibitiwa na makundi ya wapiganaji ambapo takriban miili 15 ya magaidi ilipatikana wakati wa shughuli za jeshi.
Alhamisi ya Januari 25, 2023, raia 12 waliuawa katika mashambulizi mawili huko Dassa, katikati-magharibi mwa Burkina Faso, umbali wa kilomita 140 kutoka Ouagadougou aneo ambalo limekumbwa na mfululizo wa mashambulizi mabaya huku Makao makuu ya jeshi yakitoa wito kwa raia kukatishwa tamaa na adui bali waviunge mkono vikosi vya jeshi.