Mataifa manne ya Kiarabu yameipa masharti Qatar ya kukifungia kituo cha habari cha Aljazeera na kpunguza uhusiano wake na nchi ya Iran pia na kufunga kambi ya kijeshi iliyopo Uturuki kwa kipindi cha siku kumi.
Aidha, Saudia, UAE, Misri na Bahrain kwa pamoja zimetoa masharti mengine 13 iyatimize kama inataka kuondolewa vikwazo ambavyo imewekewa na umoja huo kulingana na vyombo vya habari.
Qatar ilitengwa na mataifa hayo kwa tuhuma za kufadhili magaidi ambao wamesababisha kukosekana kwa amani katika ukanda huo, tuhuma ambazo zimekanushwa vikali na nchi hiyo.
Hata hivyo, taifa hilo lianakabiliwa na vikwazo vya kidiplomasia na Kiuchumi ambapo mgogoro huo umechukua taribani wiki mbili sasa na ikiwa ni hali mbaya zaidi kutokea katika ukanda huo.