1. Mwivi aliyelala
Tukio hili liliwashangaza wengi, likihusishwa na imani za kishirikina wengine wakisema kachanganikiwa na wengine wakidai ni uchovu baada ya kumkuta mwizi aliyelala akiwa kazini.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa mwizi huyo alikuwa amechoka baada ya kufanikiwa kuvunja nyumba huko jijini Glasgow, nchini Scotland, ambapo wenye nyumba waliporudi waliingiwa hofu kukuta mwizi wao akiwa wamelala na amejifunika shuka mtaani kwao Doritos.
Walichofanya ni kupiga simu Polisi na kutoa taarifa za tukio hilo na bada ya kufika walimfunga pingu na kumuacha hadi alipoamka na kukutana na suprise hiyo matata na mchongo wake ukaota michongoma.
2. Utajiri wa haraka
Mwanaume mmoja wa jiji la Texas, Charles Ray Fuller alibuni mpango wake wa kupata utajiri wa haraka. Alitakiwa aende kwa muhudumu wa benki ya Fort Worth na kutoa dola bilioni 360.
Fuller mwenye umri wa miaka 21 alitarajia kutumia hundi hiyo ya uwongo kupata pesa za kuanzisha kampuni yake ya kurekodi muziki na kuanzisha lebo ya Wasanii.
Akiwa amepofushwa na matamanio yake ya utajiri wa haraka, Fuller alifanya makosa kadhaa ikiwemo kuweweseka na kutojiamini hali ambayo ilizidisha hofu kwa muhudumu ambaye aliwataarifu Polisi ambao walifika eneo la tukio mara moja, wakagundua kuwa pia alikuwa na bangi na bastola, ndoto zake zikafia hapo.
3. Mhalifu kaelekeza njia
Huwezi pata jibu ni jinsi gani wachunguzi wa eneo la uhalifu na wataalamu wa Mahakama waliweza kugundua tukio la uhalifu. Kama tunavyofahamu wao wana zana nyingi za kugundua kila kitu zaidi ya macho ya mwanadamu.
Ilikuwa hivi; Mwanamume mmoja alivunja duka na hakuiba kitu chochote chenye thamani zaidi ya kuchukua kutoweka bila chochote isipokuwa kitafunwa ambacho hupendwa sana na watoto kiitwacho Chama.
Polisi walifika haraka kwenye eneo la tukio na kugundua jambo moja la kushangaza asubuhi iliyofuata. Mhalifu alikuwa ameacha mchoro wa sehemu aliyoelekea na walimfuata kwa msaada wa mtu aliyeshuhudia na kisha walimkamata akiwa anajiburudisha na vitafunwa hivyo.
4. Bomba lakwamisha dili
Mwaka 2017, mwizi mmoja alipatwa na majanga baada ya kukwama kwenye bomba la moshi. Mwizi huyo Keith Schultz, alikuwa katika misheni yake ya kutekeleza mpango wa wizi katika nyumba moja iliyopo Detroit Marekani lakini alishindwa.
Mwenzake alipogundua kinachoendelea, alianza kuingiwa na hofu na alijaribu kufanya majaribio kadhaa ya kumuokoa rafiki yake lakini akaishia kupiga kgele ya tahadhari kuomba msaada wa kiusalama na ndipo Polisi walipofika na baada ya kuhoji ilikuwaje wakakamatwa.
5. Kabati latibua mambo
Wahalifu wawili John Arwood na Amber Campbell walikuwa na saa 48 za kujiokoa baada ya kunasa kimakosa kwenye kabati la Chuo cha Jimbo la Daytona mwaka 2014.
Walitumia siku mbili kukaa ndani ya kabati la shule kabla ya kupiga simu 911 kuomba msaada, ambapo Polisi walifika eneo la tukio na kugundua kuwa mlango ulifunguliwa.
Polisi walishangaa kwa nini washukiwa wahalifu hawakukimbia lakini wakagundua ilikuwaje na ndipo wakawamakata na kuwafungulia mashitaka ya uvunjaji wa sheria.