Sina shaka unakumbuka kisa cha Bwana Paul Mackenzie ambaye alijinasibu kuwa ni Mtumishi wa Bwana, akimiliki kanisa la Good News International lililopo mji wa Pwani wa Malindi uliopo Nchini Kenya.

Bwana Mchungaji huyu  alisababisha huzuni, majonzi na vilio kwa familia, wananchi, Afrika na  Wananchi kwa ujumla kwa kuwalaghai waumini wake kuwa wanatakiwa waingie katuka mfungo wa kutokula wala kunywa mpaka watakapokufa, eti akiwaaminisha kuwa hapo watakutana ma muumba wao.

Mackenzie anasema kanisa hili alilianzisha Agosti 17, 2003 na akaweka matawi katika mikoa mbalimbali nchini kenya ikiwemo jijini Nairobi, Watamu, Malindi, Kitale, Machakos, Naivasha, Mombasa, Mwea, Lunga Lunga, Matano manne na Makao Makuu ya Dhehebu hilo aliyaweka katika eneo la Malindi Furunzi.

Anasema dhamira ya huduma 2a Kanisa lake ilikuwa ni kuwalea waamini kwa ukamilifu katika masuala yote ya kiroho ya kikristo wakati wakijiandaa kwa ujio wa pili wa Yesu Kristo kupitia mafundisho na uinjilisti huku akihubiri unabii juu ya nyakati za mwisho.

Sasa nini kilimsibu mpaka akawapeleka waumi ni wake kwenye ardhi ya shamba lake, akawaambia wafunge kula na kunywa mpaka watakapokufa ili wakutane na MUNGU wao bila kufafanua azma ya mkutano huo kati ya waumini na Muumba wao baada ya kufa?.

Hili ndilo jambo ambalo kila mtu alikuwa akijiuliza wengine wakisema “Watumishi wa aina hii wanatupeleka Wapi?.

Hapa Tanzania kuna Mchungaji mmoja maarufu anaitwa Anthony Lusekelo, al-maarufu kama Mzee wa Upako, aliwahi kusema kwamba, “wewe unaamini nini? Baki na imani yako, lakini usivunje sheria za nchi.”

Hebu tutafakari  msemo huo kwa pamoja huku ukiomba MUNGU akupe uwezo aa kutambua mabaya na mema.

Busu, kumbatio vyatajwa kuwa hatari kwa afya
Watakiwa kuishinda dhamira mbaya kukwepa uhalifu