Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amewataka watendaji wa Wilaya hiyo kubuni vyanzo vya mapato pamoja usimamizi Bora wa ukusanyaji, huku akikemea matumizi holela ya fedha mbichi na kutaka ziingizwe benki kwanza.
Shaka, ameyasema hayo katika Baraza la Madiwani Wilayani humo na kuongeza kuwa baadhi ya watendaji wa Vijiji, Kata, Madiwani na Watumishi wamekua kikwanzo cha Serikali kukomesha changamoto hiyo kwa kuchukua rushwa kwa wafugaji na wakulima.
Awali, katika kikao hicho Mwenyekiti wa baraza la madiwani Halmashuri Wilaya ya Kilosa, Wilfred Sumari alisema kinachoendelea ni uzembe, kwani tayari Serikali ilishatoa maekekezo Kila kijiji kufanyike utambuzi wa mifugo na wafugaji, kuunda kamati za usuluhishi na kuondoa mifugo ambayo imeingia bila kibali.
Alisema, tayari muda muafaka umefika kwa watumishi kuanza kuchukuliwa hatua stahiki kwani na kuepuka kuwa chanzo za changamoto hiyo, kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya Viongozi wa juu, na kusababisha uendelevu wa migogoro.