Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amezindua magari 22 ya TAWA yatakayotumika Kwa ajili ya shughuli za doria na kudhibiti Wanyamapori Wakali na Waharibifu.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa magari hayo Mkoani Morogoro, Mchengerwa amesema yatatumika katika shughuli za doria, kudhibiti ujangili na Wanyamapori Wakali na Waharibifu.

Amesema mbali na shughuli za kudhibiti ujangili, magari hayo pia yatumike katika kujenga mahusiano mazuri na Wananchi wanaozunguka maeneo ya hifadhi.

“Nitataka Kila mmoja wetu akafanye kazi kwenye eneo lake, na afanye kazi kwelikweli, kama utatakiwa kuwepo kwenye eneo lako Saa sita mchana uwepo kwenye eneo lako” amesisitiza Mchengerwa.

Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri Mchengerwa tangu kuteuliwa na Rais Dkt. Samia kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na katika Ziara yake aliongoza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas Said.

Wengine waliongozana na Waziri Mchengerwa ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Juma Mkomi, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Prisca Lwangili na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha.

Rais athibitisha kujiuzulu kwa Makamu wake
Ukandamizaji haki: Wanahabari, Wanaharakati waungana