Polisi mkoani Mbeya inawashikilia watu wawili, Mwalimu wa shule ya sekondari Loileri ya Mbalizi, Peter Emmanuel (29) na mlinzi wa Shule hiyo, Haruna Issa (30), kwa tuhuma za kumshambulia kwa viboko sehemu mbalimbali za mwili mwanafunzi wao wa kidato cha nne, Laurance Nicholous.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema Mwanafunzi huyo anaendelea kupatiwa matibabu baada ya kushambuliwa akituhumiwa kuiba maandazi, katika duka la shule.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga akitoa taarifa juu ya tukio hilo.

Amesema, Mwanafunzi huyo amepata majeraha sehemu ya paji la uso, mkono wa kushoto na kwenye magoti yote mawili na kueleza kuwa baada ya kumshambulia na kumjeruhi mwanafunzi Mwalimu na mlinzi walimpeleka hospitali teule ya Ifisi, kwa matibabu.

Hata hivyo, Kamanda Kuzaba amesema upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea na watuhumiwa watafikishwa Mahakamani, mara baada ya upelelezi kukamilika.

Burna Boy afunguka mazito sakata la kifo cha 'AKA'
TASAF Malinyi yatoa zaidi ya Mil. 80 kwa kaya masikini