Zaidi ya shilingi Milion 80, zimetolewa na Mfuko wa kunusuru kaya masikini 3258 za Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, kwa kipindi cha malipo ya dirisha la Novemba na Desemba 2022

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa TASAF Wilayani Malinyi, Sylvia Lussumo ambaye amesema kiasi cha Shilingi Milioni 54.6 yamefanyika kwa njia ya taslim na Shilingi Milion 25.5 zimelipwa kwa njia ya mtandao na Benki.

Baadhi ya walengwa wa mradi wa TASAF.

Amesema, kati ya walengwa 3258 walengwa 2559 wanaendelea kushiriki kufanya kazi katika Miradi ajira Muda 31 katika vijiji ambapo wanatarajia kupokea malipo ya Ujira katika dirisha la January- February 2023.

Miradi hiyo inayotekelezwa ni pamoja na Miradi kuboresha miundombinu ya Jamii, ukiwemo ule wa ujenzi wa barabara na Vivuko.

Wizi wa Maandazi: Mwalimu, Mlinzi mbaroni kwa shambulizi
Mauaji na ukatili: Polisi yaja kivingine