Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bodi na Menejimenti ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Rais Mwinyi ametoa pongezi kwa mamlaka hizo za Serikali kwakuona umuhimu wa ujenzi wa Ofisi na maabara inayolenga kuimarisha huduma za Nguvu za Atomu Zanzibar.

Amesema, Uwekezaji huu utaimarisha udhibiti wa matumizi salama ya mionzi pamoja na kuimarisha utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Pongezi hizo zimetolewa na Dkt. Mwinyi wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania(TAEC), zilizopo eneo la Dunga Zuze, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Dkt. Kimei: Wapinzani msipinge kila kitu, CCM haina ubaguzi
Mbatia, Mrema hawakufanya kitu Vunjo: Dkt. Kimei