Serikali nchini katika mwaka wa fedha 2022/2023
imepanga kutoa mitungi 100,000 bure ifikapo Julai 2, 2023  katika maeneo ya Vijijini vyote ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi.

Mkurugenzi wa Uenezaji Masoko na Teknoloji, Wakala wa Nishati Vijijini – REA, Mhandisi Advera Mwijage ameyasema hayo wakati  akizungumza na Wadau wa gesi nchini na kuongeza kuwa tayari wameanza kuweka fomu ya maoni kuhudu mpango huo.

Amesema, nishati safi ni ile isiyochafua mazingira, ambayo inalinda afya ya mtumiaji ambapo pia Serikali inataka kuhakikisha Wananchi wote wanafikiwa na nishati hiyo kwa uhakika.

Hata hivyo, hatua hiyo, imefikiwa baada ya Serikali kupitia kwa Wakala wa Nishati Vijijini – REA, kutenga kiasi cha Shilingi 3.2 Bilioni kwa  kwaajili ya usambazaji wa gesi hiyo safi ya kupikia.

Mayele aunguruma Singida, alama tatu lazima
Hatari ya kifo: Marufuku kutembea nje kwa saa 58