Gwiji ni Yule mtu ambaye ameleta mafanikio kwa kitu Fulani kwa kukkisaidia kufika mafanikio. Ila kisoka ukisema gwiji ni Yule mtu ambaye ameisaidia timu kubeba vikombe au kufikisha mafanikio hata kuipeleka fainali mfano wa magwiji Abdalah King Kibandeni, Pele, Sunday Manara “computer” na wengine uwajuao

Mei 17, 2012 Simba SC ilimpoteza kiungo wake mahiri aliyeisaidia kumfunga mtani wake Yanga goli Tano kwa bila (5-0) Mungu akulaze panapostahili Patrick Mutesa Mafisango mchezaji wa Simba SC na si gwiji kwani uliisaidia klabu yako kumfunga Yanga 5 tu labda na kubeba mbuji kwa msimu huo.

Ismail Aden Rage alisema uongozi wa Simba umekubaliana kutoitumia jezi namba 30 iliyokuwa ikitumiwa na kiungo huyo ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu yake ila hakuonyesha muda gani jezi hiyo kutotumika.

Marc Vivien foe jezi yake namba 23 katika klabu ya Man city Ilistaafishwa na Manager wa kipindi hicho Kevin Keegan.Alifariki akicheza uwanjani kati Cameroon na Colombia. aliisaisaidia Cameroon kufika fainali japo yeye alifariki dakika 72. Lakini katika klabu ya Man City jezi hiyo haivaliwi ila si ajabu siku moja ukaona imevaliwa jezi namba 23.

Katika taifa lake la Cameroon jezi yake namba 17 inatumika si ajabu sababu hiyo nayo pia ni sehemu ya kumuenzi mchezaji huyo na si gwiji kama utakavyomtaji labda Pele au Edward Chumila.

Mafisango hakuwa gwiji kama tunavyodhani mana hadi inafaikia hatua na mashabiki na wanasimba kwa ujumla wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wao Ismaili Aden Rage kuona Mseja kutumia jezi hiyo ni mkosa.

Simba endeleeni kushikilia vitu vya kuiga bila kuwa na uchunguzi navyo mmeshindwa hata kustaafisha jezi aliyotumia Kibandeni si alimfunga Yanga goli 3 peke yake na mkashinda 6-0 mwaka 1976 hayo hamuyaoni.

Mnajivunia kushiriki fainali ya Caf 1993 mbona mnawasahau waliowafikisha huko Malota Soma ambaye leo ni dereve Taxi, marehemu Ramadhani Reni na Edward Chumila na hata Mwenyekiti wa kipindi hicho Marehemu Ally Amri Bamchawi hamkustaafisha jezi zao wala kuwakumbuka kwa namna yoyote wakati ndio magwiji wanaopaswa kukubukwa.

Klabu kila siku wakisajili mchezaji wanataka kumfananisha na Marehemu Mafisango si haki hata kidogo mana alishafariki mwacheni apumzike kwa amani angalieni mbele.

Alifaririki Antonio Jose Puerta ambaye aliisaidia Sevila kubeba Copa De Rey, Super Copa De Espana na kufika Uefa mwaka 2007 ila jezi yake ilistaafishwa na tukaiona tena Federico Fazio kaitinga uwanjani namba 16 hata katika klabu yake David Prieto aliitumia kama ndo hivyo Mheshimiwa Ismaili Rage naomba nitajie makombe aliyoisaidia Mafisango kuyachukua nna hakika hayafiki hata 3.

Wachezaji wameaminisha hilo wakifunga bao wanenda kutoa saluti kwenye picha ya Mafisango si jambo baya ila mnawanyima haki wale ambao na wao walifanikiwa kuliko Mafisango na hamuwafanyii hivyo kama ni kumfunga mtani mnaweza kuendelea na imani yenu ilas sidhani kama ni suluhisho kuhusisha jezi ya Mseja na kifo cha Mafisango.

Mnahisi hiyo ndo itakuwa salam yenu kuepuka kuambiwa mmekula rambirambi la hasha bali mtabaki kumkumbuka mchezaji na si gwiji kama mnavyozani

Aden rage muheshimiwa kila ulifanya vizuri ila si jambo kubwa sana jezi ya mafisango kurudi tena uwanjani nayo pia ni njia mojawapo ya kumuenzi Mafisango tena jezi  inavaliwa na golikipa chipukizi Emmanuel Mseja.

Mungu awapumzishe kwa amani Edward Chumila, Patrick Mutesa Mafisango, Ramadhani reni,Ally Amri Bamchawi, Alex Christopher na wengine wote.

Imeandaliwa na Annasi S. Mlangi.

Serikali yatoa shilingi bilioni 24.4
Ronaldinho Gaucho astaafu soka