Timu za Simba na Yanga zimeruhusiwa kuanza kuutumia Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa baadhi ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na zile za kimataifa zilizo chini ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).

Simba ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuufungua uwanja huo katika mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Singida United utakaopigwa Alhamisi Januari 18 mwaka huu, huku Yanga wakiutumia Jumapili watakapokabiliana na Ruvu Shooting.

Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amesema hatua hiyo imetokana na jitihada za bodi hiyo kuiomba Serikali ambao ndiyo wamiliki wa uwanja huo, ambao wameziruhusu timu hizo kuutumia mara moja pekee kwa wiki.

“Wamiliki wa uwanja wametoa ruhusa utumike kwa mchezo mmoja pekee kwa wiki, lakini bado tunaendelea kuzungumza nao ili ikiwezekana watuongezee,” amesema Wambura.

Wambura amesema mechi nyingine zinazohusu timu hizo zitaendelea kutumia uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Serikali iliufungia uwanja huo tangu mwezi Septemba mwaka jana kwaajili ya matengenezo ambayo tayari yamekamilika.

Ronaldinho Gaucho astaafu soka
Okwi aomba msamaha, kocha Irambona amsamehe