Zoezi la awamu ya tatu, ya upasuaji na uchunguzi wa miili nane kati ya iliyoondolewa kwenye makaburi yaliyofukuliwa katika msitu wa Shakahola, imekamilika katika hifadhi ya maiti ya Hospitali Kuu ya Malindi nchini Kenya huku miili 117 kati ya 338 iliyopasuliwa ikiwa ni ya watoto.

Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali, Dkt. Johansen Oduor amewaambia Waandishi wa Habari kuwa mtu mmoja aliyefariki katika gezera hivi majuzi hajafanyiwa upasuaji, kutokana na taratibu za familia juu ya utambuzi wa marehemu huyo, kabla ya kuendelea na uchunguzi.

Amesema, “tangu kuanza kwa shughuli ya upasuaji katika awamu zote tatu, tumefanya upasuaji wa miili 338, miili 201 ikiwa ya watu wazima, miili ya watoto ikiwa 117 huku miili mingine 20 ikishindikana kutambulika wahanga walikuwa na umri gani. Hii ni kwa sababu miili hiyo ilikuwa imeharibika.

Katika zoezi hilo, imebainika kuwa watu wawili waliuawa kwa kupigwa nyuma ya kichwa, watatu walifariki kutokana na ukosefu wa maji na chakula, huku wengine watatu chanzo cha vifo vyao kikiwa hakikubainika.

Kevin De Bruyne awekwa pembeni Man City
Kakolanya: Moses Phiri ni zaidi ya Mayele