Jumla ya Askari Polisi sita wameuwawa katika shambulizi la kushtukiza lililotokea aneo la Kaskazini Magharibi mwa Pakistan, ambapo kundi la Taliban nchini humo limekiri kuhusika na kuleta simanzi kwa familia za marehemu.
Washambuliaji waliojihami kwa bunduki, waliliwamiminia risasi Polisi waliokuwa kwenye gari wakitimiza majukumu yao ya doria, katika kijiji cha Shahab Khel kilichopo kilomita 100 kutoka mpaka wa Aghanistan eneo ambalo limekuwa na mashambilizi ya kushtukiza.
Afisa wa Serikali katika Mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, Tariqullah Khan amesema Polisi wote sita waliuwawa katika shambulio hilo huku Waziri Mkuu, Shehbaz Sharif akitoa salamu za rambirambi na kusema ugaidi unaendelea kuwa moja ya matatizo makubwa ya Pakistan.
Kundi la Taliban la Pakistan, lililo na mafungamano na kundi la Taliban la Afghanistan, limekuwa likitekeleza mashambulizi kadhaa tangu mji wa Kabul ulipotawaliwa na kundi hilo, lililo na itikadi kali linalosimamia majukumu yake kwa misimamo.