Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amewataka Mawakili wapya kuzitumia fursa zilizopo kujiajiri badala ya kusubiri ajira.
Ametoa ushauri huo hii leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili wapya 296 waliohitimu shule ya sheria.
“Niwashauri Mawakili wapya, anzeni kufanya kazi, Itashangaza sana na nitawashangaa sana kama na nyie mtakaa mtaani mkisubiri kuajiriwa badala ya kutumia taaluma na ujuzi mlioupata kujiajiri wenyewe,”amesema Masaju
Mhe. Masaju amewataka mawakili hao kwenda mikoani na wilayani ambako amesema, kuwa kuna fursa nyingi za kujiajiri na pia kuna wateja wengi wenyeuhitaji mkubwa wa kupata huduma ya za kisheria.
Aidha, amesema kuwa kwa watakaobahatika kuajiriewa kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Utumishi wa Umma watapaswa kuzingatia ipasavyo Maadili ya Msingi yanayosimamia utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
-
TWAWEZA: Asilimia 46 ya walimu wa Shule za Msingi hawahudhurii Shuleni
-
Video: Kama vyuma vimekaza wekeni grisi- JPM, Mwaka 2017 wapinzani wamevugwa
-
Kamanda wa Polisi Arusha athibitisha kutokea kwa kifo cha Askari Magereza
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma na Makamu wa Raisi wa Chama cha Mawakili Tanganyika ( TLS) Godwin Simba Ngwilimi wamewataka Mawakili hao kuzingatia maadili ya kazi yao kwa pamekuwepo na malalamiko mengi ya ukiukwaji wa maadili.