Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi, kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo, unaofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha unajadili masuala mbalimbali ya utangamano wa Jumuiya hiyo, pamoja na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa ViwandaBiashara, Dkt. Ashatu Kijaji, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil na Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba.
Wengine ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata, Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Elijah Mwandumbya na Maafisa waandamizi wa Serikali kutoka baadhi ya Wizara.