Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande wameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwashughulikia watumishi wanaotoa vitisho, ubabe na wanatengeneza mazingira ya kupata rushwa kutoka kwa wafanyabiashara.
Wameyasema hayo wakati wa hafla ya maadhimisho ya kilele cha wiki ya mlipakodi mwaka 2022 iliyoambatana na utoaji wa tuzo kwa walipakodi bora.
Kauli za viongozi hao zimekuja siku chache tangu Mwenyekiti wa bodi ya TRA, Uledi Mussa atangaze mamlaka hiyo kukiondoa kikosi kazi cha kukusanya kodi wakati akizungumza na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Hata hivyo TRA imetakiwa kutathimini utendaji wake kutokana na malalamiko ya kuwakadiria kodi kubwa wafanyabiashara, kutoza kodi kabla ya biashara kuanza na urasimu kwenye ulipaji wa kodi.