Akount ya Twitter ya Rais wa Zamani wa Marekani Donald Trump imerejeshwa na mmiliki wa kamapuni hiyo na boss wa Tesla Elon Musk, ambapo wafuasi wa mtandao huo wamepiga kura ya kurejesha akaunti hiyo.

Akaunti hiyo, ambayo ilifungiwa kufuatia shambulio la Januari 6, 2021, kwenye Capitol, imerejeshwa baada ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Twitter na mmiliki mpya kuhoji watumiaji wa Twitter ikiwa Trump anafaa kurejeshwa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Musk ameandika, “Watu wamezungumza. Trump atarejeshwa,” “Vox Populi, Vox Dei,” akaongeza kwa kilatini akimaanisha “Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.”

Kwa mujibu wa kura zilizopigwa mpaka kufikia asubuhi ya leo Novemba 20, 2022 asilimia 51.8 ya kura milioni 15 zilizopigwa kwa siku mbili zilitaka Trump arejeshwe. Asilimia 48.2 ya kura hizo hawakutaka Trump arejee katika jukwaa hilo.

Uamuzi huo unaweka mazingira ya kurejea kwa rais huyo wa zamani kwenye mtandao wa kijamii ambapo hapo awali alikuwa na ushawishi mkubwa zaidi, ikiwa ni mtumiaji mwenye utata.

Akiwa na karibu wafuasi milioni 90, tweets zake mara nyingi ziliweka mzunguko wa habari na kuendesha ajenda huko Washington.

Akaunti inayoonekana kwa sasa ni ya @realDonaldTrump ikiwa na wafuasi milioni1.

Itakumbukuwa kuwa Trump alisema angesalia kwenye jukwaa lake, Truth Social, badala ya kujiunga tena na Twitter, lakini mabadiliko katika mtazamo wake yanaweza kuwa na athari kubwa za kisiasa.

Rais huyo wa zamani alitangaza mwezi huu kwamba atawania uteuzi wa urais wa Republican mwaka wa 2024, akilenga kuwa kamanda mkuu wa pili kuwahi kuchaguliwa kwa mihula miwili tofauti.

Mawaziri waonya wanaotoa vitisho TRA
COP27 yaidhinisha mfuko wa kuzisaidia nchi maskini