Nahodha na Kiungo wa Zamani wa Young Africans Ali Mayai ameingilia kati sakata la aliyekua Msemaji wa Simba SC Haji Manara dhidi ya Mwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’ na Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez.

Mayai ambaye ni Mwajiriwa wa Serikali na pia Mchambuzi wa Soka la Bongo amewasilisha andiko lenye hoja, ambalo ni kama linajibu madai ya Haji Manara alioyatoa alipozungumza na Wanahabari mapema juma hili.

Mayai ameandika: Manara anasema Barbara ndo chanzo Cha watu wengi kufukuzwa pale Simba na hapohapo anasema Senzo alipokuja aliambiwa amfukuze, kumbuka Kabla ya Senzo CEO wa kwanza Simba ni Crisentus John Magori.

Sasa wakati Senzo anakuja Barbara hakuwa na nguvu yoyote kwenye bodi ya wakurugenzi wa Simba na mwenyekiti alikuwa “Try Again” sasa kama Senzo aliambiwa amfukuze kazi maana yake bodi tangu awali ilikuwa haimkubali? Na ilishindikana nini kufukuzwa?

Yaani Senzo aliivimbia bodi ya Wakurugenzi wa Simba akashindwa kumfukuza Manara? Za kuambiwa changanya na zako.

Manara anasema analipwa laki 7 (700,000/= per month) fine, ila anakili kupewa mkataba wa million 3 kama si nne wenye masharti ya kutotangaza bidhaa za GSM na Bakheresa. Sasa ni mkataba gani wa kazi usiyo na masharti?

Manara anasema alikuwa hakatiwi tiketi kwenda mechi za mikoani, sawa. Kwani alikuwa na umuhimu mkubwa kuhudhuria mechi za Simba za mikoani? Kama ndiyo, kwanini mechi nyingi za Simba za Dar es Salaam alikuwa haji uwanjani? Umuhimu wake ulikuwa mechi za mikoani kuliko mechi za Dar es salaam?

Yote kwa yote Manara anaweza kuwa na hoja sahihi ila si yoote aliyosema. Na aache kupenda kutafuta huruma ya mashabiki.

Ajifunze kubadilika kulingana na nyakati. Zama za ujanjaujanja zimepita. Atambue mashabiki wanataka kuona Mpira ukichezwa na timu yao ikifanya vyema.

Sasa kunyamaza ni njia sahihi kwake haijalishi anaongea ukweli au uongo kuchafua viongozi na kutafuta huruma ya mashabiki.

Wasalaam,

Ali Mayai
Safarini Uyui

Usajili CAF: Biashara United Mara bado kizungumkuti
'Mo' apewa mbinu za kuzima kelele mitandaoni