Klabu za Simba SC, Young Africans, Azam FC na Biashara United Mara, zimesaliwa na muda wa juma moja kukamilisha usajili wa wachezaji kwa ajili ya Michuano ya Afrika itakayoanza rasmi mwezi ujao.

Klabu hizo nne zitaiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Vilabu msimu ujao, ambapo Simba SC na Young Africans watacheza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika huku Azam FC na Biashara United Mara zikitarajia kushiriki Kombe la Shirikisho CAF.

Muda wa usajili kwa timu shiriki kwenye michuano hiyo ya Vilabu utakoma Agosti 15, ili kupisha taratibu nyingine za amaandalizi kuendelea ndani ya CAF.

Leo ni Agosti 07, kimahesabu zimesalia siku 8 dirisha la usajili la kimataifa kufungwa kwa vilabu vya Tanzania, lakini bado klabu ya Biashara United Mara imeendelea kuwa kimya.

Kwa upande wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, wameshakamilisha usajili na kinachoendelea kwa sasa ni kutangaza majina ya wachezaji waliowasajili.

Azam FC bado wa nafasi moja ya mchezaji wa kimataifa, baada ya kusajili kwa ubabe ndani ya majuma mawili yaliyopita.

Young Africans bado wana nafasi mbili za usajili wa kimataifa ili jeshi lao likamilike, ila kwa Biashara United Mara ndio shida kuna haja ya TFF kuwakumbusha na kuwasaidia katika hili isije ikafika tarehe 14 ndio waanze kuhaha masuala kusubili deadline sio mazuri.

Kwa upande wa maandalizi, klabu hizo nne za Tanzania zinapaswa kuanza kujiandaa mapema kwani mashindano ya Afrika yanatakiwa kuanza September 10-12 kwa michezo ya mkondo wa kwanza kwa raundi ya awali (preliminary) na ratiba (draw) nzima ya mashindano ya CAF itatolewa August 15.

CAF imeendelea na utaratibu wa timu kufanya mabadiliko (sub) ya wachezaji watano (5) kwenye mchezo mmoja badala ya watatu (3) pia kwenye bechi wanaruhusiwa kukaa wachezaji tisa (9) badala ya wachezaji saba (7) na kwenye usajili timu inaruhusiwa kusajili wachezaji wasiozidi 40 badala ya wachezaji 30.

Mzaha ulivyomponza mtumishi wa serikali
Mayai aingilia kati sakata la Manara na waajiri wake wa zamani