Bondia mstaafu, tajiri Floyd Mayweather ameweka picha mbalimbali kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akionyesha jinsi anavyoponda raha za maisha yake ya kustaafu.

Picha hizo zimekuwa zikionyesha ziara mbalimbali katika nchi tofauti tofauti.

Bondia huyo mstaafu hivi karibuni alikuwa nchini Uturuki na sasa yupo nchini Ufaransa.

Kwa sasa Mayweather anazunguka pande mbalimbali za dunia akiwa na chopa yake ambapo alitoka Istanbul na kwenda Ufaransa.

Akiwa Uturuki alikutana na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Lukas Podolski.

Lionel Messi Auenzi Msaada Wa Ronaldinho
FBI Walivalia Njuga Suala La Babu Blatter