Mbunge wa Iringa mjini, Jesca Msambatavangu amewaasa Wananchi kuyalinda na kuyatunza mazingira yanayowazunguka na kusema faida za Mazingira ni kwa ajili ya wanajamii wote si Serikali peek yake kama baadhi ya watu wanavyofikiri.

Msambatavangu ameyasema hayo mjini Iringa Mara baada ya kupokea zawadi ya kumbukumbu ya picha, aliyopatiwa na uongozi wa Dar24, na kuwasilishwa kwake na Mtangazaji na Mwandishi wa Habari, Stanslaus Lambat.

Amesema, “Serikali na Wadau wa Mazingira tunapopiga kelele juu ya utunzaji na uhifadhi wa Mazingira hatufanyi hivyo kwa ajili yetu sisi au kwa manufaa ya mtu fulani hapana,  hiyo in kwa ajili yetu sote na kwa maisha ya vizazi vijavyo.”

Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu wakati akiongelea suala la utunzaji na uhifadhi wa Mazingira.

Aidha, Mbunge huyo amebainisha kuwa vyanzo vingi vya maji na ukosefu wa mvua za uhakika umekiwa ukisababishwa na baadhi ya watu wasio waaminifu kuharibu vyanzo na ukataji wa miti hovyo, kite ambacho hakifai na kinapaswa kukemewa.

“Watu wanalalamika kuhusu mgao wa umeme, uhaba wa mvua wengine kukosa mazao kwa uhakika, sababu ni uharibifu wa Mazingira maana mabwawa yanayochangia uzalisha wa umeme yamekauka au kupungua maji tujirekebishe,” amebainisha Msambatavangu.

Serikali, kupitia mamlaka mbalimbali na wadau wa Mazingira wamekuwa wakipaza sauti juu ya suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira, huku vyombo vya Habari ikiwemo Dar24 vikiendelea kuuhabarisha, kuuelimisha na kuutaka umma kupambania kwa mfumo chanya juhudi za kulinda mazingira.

Waandamana kupinga safari nyingi za Rais nje ya nchi
Waliofariki kwa mafuriko DRC wafikia 160