Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amezindua Maonesho ya Wafanyabiashara Mkoani Manyara ‘Tanzanite Manyara Trade Fair’ ambayo yameandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Nchini – TCCIA, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara na mdhamini Mkuu Kampuni ya MATI Super Brands Ltd.

Kagahe amezindua maonesho hayo hii leo Oktoba 18, 2023 na kuutaka Mkoa wa Manyara kushirikiana na Waratibu wa TCCIA kusogeza huduma karibu kwa Wajasiliamali, washiriki wa maonyesho na Wananchi na kuongeza kuwa Taasisi za Serikali na binafsi zikiboresha mazingira ya uwekezaji zitatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza kwa kuzalisha bidhaa zitakazopata soko la Dunia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Manyara, Musa Msuya ameshukuru Serikali kwa kukubali kujenga Kiwanja cha Ndege katika Mkoa huo, kwa kuwa utaongeza idadi ya wawekezaji na watalii na kuongeza kipato cha mkoa.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya MATI Super Brands Ltd, Elvis Peter amewashukuru TCCIA Kwa kuandaa maonesho hayo na kusema wataendelea kuwaunga mkono kwani wapo kuisaidia jamii katika mambo mbalimbali, huku Mfanyabiashara, Ester Chessa akiwashukuru waandaaji kwa kuwapa fursa ya kuonesha bidhaa zao na kutambulika Kwa ujumla.

Thiery Henry: Huyu Messi ni balaa
Miguel Gamondi: Azam FC watatusamehe Jumapili