Wakulima wa zao la mbaazi ghafi Mkoani Lindi, wamepata Sh bilioni 32.8 msimu huuambapo kwa miaka ya nyuma ya nyuma wakulima wa zao hilo walikuwa wanauza mbaazi ghafi kwa Sh 2000 kwa kilo moja.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack hii leo Septemba 18, 2023 wakati akitoa taarifa ya Mkoa mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye mkutano wa hadhara wa kuweka Jiwe la Msingi katika barabara itokayo Nanganga Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara hadi Ruangwa Lindi.
Amesema, mauzo hayo yalitokana na kukubaliana na Wizara ya Kilimo kwa kuridhia kuuzwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kilo moja iliangukia Sh 2000 hadi Sh 2005.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa, pia zao la ufuta liliweza kuwapatia wakulima Sh bilioni 98 msimu huu, huku zao la Korosho likiuzwa kwa Shilingi bilioni 106 msimu uliopita.
Hata hivyo amesema Mkoa Ulikiwekea mkakati wa kuzalisha zaidi mazao hayo na kuongeza kuwa ile tabia ya kusema kuwa zao la mbaazi ni mboga sasa imebadilika kwani ni zao biashara.