Uongozi wa Ihefu FC umefikia makubalino ya kumsajili aliyekuwa beki wa kulia wa Mbeya City, Kenneth Kunambi kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kumalizana rasmi na timu hiyo iliyoshuka daraja.

Ihefu FC imetumia nafasi hiyo kumpata nyota huyo baada ya kuondokewa na Nicolas Wadada aliyejiunga na Singida Fountain Gate.

Taarifa kutoka ndani ya viongozi wa Ihefu FC zinaeleza makubaliano kati yao na mchezaji yamekubaliwa na kilichobaki ni kumtangaza tu kama nyota wao mpya wa msimu ujao.

“Ameungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya msimu, ni beki bora sana na hakuna asiyejua uwezo wake hivyo kwetu ni mbadala sahihi wa Wadada,” kimesema chanzo hicho.

Kenneth Kunambi akiwa na Baraja Gamba Majogoro

Katibu Mkuu wa Ihefu, Zagalo Chalamila amesema kwa upande wao kama viongozi tayari kwa asilimia 100 wamekamilisha usajili wote ambao benchi lao la ufundi ulipendekeza kwa ajili ya msimu ujao.

Kunambi anaungana na mastaa wengine wapya wakiwemo Jofrey Manyasi aliyetokea Geita Gold, Charles Ilanfya, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ (Mtibwa Sugar) na Mcameroon, Moubarack Amza aliyetokea Coastal Union.

Wanaotoa Vitambulisho vya Taifa kwa wageni wasakwa
Jude Bellingham ampagawisha Ancelotti