Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatarajia kutumia barabara za mabasi yaendayo haraka (BRT) katika mkakati wake mpya wa kuanzisha mabasi ya umeme katika jiji la Dar es Salaam.

Akiwa ziarani nchini Ufaransa, Rais Samia ameshuhudia Tanzania ikipata zaidi ya Euro milioni 178 kwa ajili ya kuendeleza mpango wa Mwendokasi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

“Tulifanya mazungumzo kidogo wakaniuliza, kwanini haiwezekani Dar es Salaam ama Dodoma mkawa na mabasi ya kwenda kwa umeme … nikawaambia hilo linawezakana sana. Kwa hiyo hilo liko katika mazungumzo,” alisema Rais Samia baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Tulikuwa na mradi wa kujenga viwanja vya ndege nadhani za Kigoma, Shinyanga na Pemba, Pia kulikuwa na mradi wa Green Cities kwa mikoa ya Kigoma, Pemba na mji mwingine, pesa zao zilikwama lakini tulishakwamua, mradi mmoja umeshatiliwa (kutia saini) na mwingine utatiliwa hivi punde,”amesema

Pia, Rais Samia amefanikiwa kupata fedha kwa ajili ya kumalizia njia za Miradi ya Mwendokasi  pamoja na shughuli za Kilimo.

Watoto 7 wauwawa kwenye Shambulio la anga Niger
Makamu wa Rais Dkt Mpango aifariji familia ya Malecela