Utafiti unaonyesha kuwa mbegu ya parachichi inakiwango cha asilimia 65 cha amino acids na pia ina kiwango kikubwa cha fiber ukilinganisha na vyakula vingine.
Watumiaji wengi wa parachichi hawafuatilii tunda lililopo katikatika ya parachichi ambalo lina faida katika mwili wa mwanandamu.
Mbegu ya parachichi huweza kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘antioxidants’ hii ni kutokana mbegu hiyo na kuwa na zaidi ya asilimia 70 ya kirutubisho hicho.
Aidha Mbegu hii ya parachichi pia huweza kuwasaidia wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito kwani matumizi ya mbegu hiyo husaidia kuunguza mafuta mwilini na hivyo kupunguza uzito mkubwa mwilini.
Matumizi ya unga wa mbegu hizo pia husaidia kupunguza shida ya maumivu ya mwili hasa kwenye maungio yaani ‘joint’ za mwili.
Pia mbegu za parachichi husaidia kurekebisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula tumboni.