Baada ya kuiadhibu Simba Sc katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Mathias Lule, ameitumia salamu Young Africans kuelekea mchezo wa Februari 05.

Young Africans itakuwa mwenyeji wa mchezo huo, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, huku ikijivunia rekodi ya kutopoteza mchezo wa Ligi msimu huu.

Kocha Lule ametoa tahadhari hiyo huku kikosi chake kikiiweka Mbeya City katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 22 kibindoni huku ikiwa imeshuka uwanjani mara 13 ikiwa juu ya Azam FC kwa alama moja.

Kocha Lule amesema kuwa malengo yao ni kushinda mchezo dhidi ya young Africans ili kufikia mkakati wao wa kuwa timu zitakazomaliza katika nafasi za juu kwenye msimamo, ambazo zitapata nafasi ya kushiriki Michuano ya Kimataifa msimu ujao.

Amesema anaamini endapo watapata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa, wachezaji wake watakuwa na fursa ya kupata uzoefu wa michuano hiyo kama ilivyokuwa kwa Namungo FC na Biashara United Mara, ambazo kwa misimu ya karibuni zimeiwakilisha nchi sambamba na Simba SC.

“Tunapaswa kuwa na muendelezo mzuri katika michezo minne ijayo ili kujiwekea katika mazingira mazuri yakutimiza malengo yetu ambayo yatatimia kama tutapata ushindi kwenye michezo yetu,” amesema Lule.

Huenda Kocha Lule amepata jeuri ya kutuma ujumbe young africans, baada ya kuibanjua Simba SC 1-0, katika mchezo wa Ligi Kuu majuma mawili yaliyopita.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 35, ikishuka dimbani mara 13.

Rihanna aonesha ujauzito wake
Rais awaapisha viongozi aliowateua