Timu ya Mbeya City FC imekua ya kwanza kukubali kufungwa mabao mengi, baada ya kuanza kwa msimu huu 2020/21 jana Jumapili kwenye viwanja sita tofauti.
Mbeya City ilicheza mchezo wake kwenye Uwanja wa ugenini dhidi ya KMC FC majira ya saa nane mchana jijini Dar es salaam, na kukutana na kichapo cha mabao manne kwa sifuri kutoka kwa KMC FC.
Mabao ya KMC FC katika mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Uhuru, yalipachikwa dakika ya 21 kupitia kwa Israel akimalizia pasi ya Emmanuel Mvuyekule.
Bao la pili lilipachikwa dakika ya 39 na Hassan Kabunda kwa pasi ya Israel na kuwafanya KMC FC kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabaomabao mawili kwa sifuri.
Kipindi cha pili KMC FC waliendeleza moto wao ambapo dakika ya 57, Abdul Hilary alipachika bao la tatu kwa pasi ya David Bryson na msumari wa mwisho ulipachikwa na Paul Peter dakika ya 74 kwa pasi ya Kabunda.
Kabunda na Israel wametaka leo Uwanja wa Uhuru ambapo wote wamefunga bao mojamoja sawa na idadi ya pasi ambazo wametoa.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliochezwa leo Septemba 07, ulikua kati ya Kagera Sugar waliokua nyumbani Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera wakiwakaribisha JKT Tanzania.
Dakika 90 za mpambano huo zimekamilika kwa wenyeji kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri, lililofungwa na Adam Adam dakika ya 16.
Mchezo mwingine unatarajiwa kuchezwa mishale ya saa moja usiku kati ya Azam FC dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es salaam.