Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa ametoa angalizo kwa watu wanaleta chokochoko na kuondoa utulivu uliopo miongoni mwa jamii na kuwataka kuacha mara moja vitendo hivyo kwani Mbeya ni kitovu cha amani na Biashara.

Malisa ameyasema hayo wakati wa mahafali ya kuhitimu kwa mafunzo ya Jeshi la akiba (Mgambo), yaliyofanyika katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.

Amesema, wanaodhani kuwa Mbeya ni kitovu cha vurugu wanatakiwa kujitathimini kwani Wanambeya hawatokuwa tayari kupoteza muda kuhatarisha amani iliyopo na Serikali ipo imara kulinda kwa maslahi ya Wananchi.

Aidha, Malisa amezitaka taasisi za Ulinzi Wilaya ya Mbeya, kuwatumia Vijana hao wahitimu mafunzo katika shughuli za ulinzi kwa kuwapatia ajira na kuacha kutumia Askari wasiokuwa na mafunzo katika taasisi zao.

Polisi waonesha upendo kwa Walimbwende Miss Tanzanite
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 7, 2023