Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka Watendaji na Wenyeviti Jijini Mbeya, kuepuka na kutojihusisha na migogoro ya Ardhi katika maeneo yao.

Malisa amesema hayo akiwa Iduda Jijini Mbeya kwenye zoezi la utoaji wa Elimu na kusikiliza kero za Wananchi zinazohusiana na masuala ya Ardhi katika eneo hilo.

Amesema, zoezi hilo linalenga kuondosha migogoro ya Ardhi Wilaya ya Mbeya, ambapo Maafisa Ardhi wa Halmashauri zote mbili za Mbeya DC na Mbeya Jiji, huzungumza na wananchi kufaham kero zao na kuzitatua.

Malisa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya amekuwa na utaratibu wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi ikiwemo za Maji, Elimu, Ardhi nk.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 30, 2023
Mkataba Euro Milioni 36 mradi wa Umeme Kakono wasainiwa