Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CADEMA), kimefanya mkutano wake wa kwanza wa kisiasa baada ya marufuku iliyowekwa mwaka 2006 kuondolewa, huku Mwenyekiti wake Freeman Mbowen akikana ”kulambishwa asali’.
Akihutubia maelfu ya wafuasi wa CHDEMA, Mbowe amekiri kusikitishwa na tuhuma hizo ambapo Mkurugenzi wa mawasiliano na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema akisema haikuwa rahisi.
Katika mkutano huo, ambao ulifanyika kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza ajenda ya uwepo wa katiba mpya ilichukua nafasi ya juu na viongozi wote waliopewa nafasi ya kuhutubia hadhira, waligusia suala hilo.
Awali, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Peter Msingwa alisema ni aibu kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuzungukwa na Ziwa Victoria, huku wakilia juu ya shida ya maji na changamoto mbalimbali.
Januari 3, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.tSamia Suluhu Hassan alitangaza kuondoa zuio la kufanyika kwa mikutano ya vyama vya siasa nchini, na CHADEMA imefungua pazia hilo rasmi siku ya Jumamosi (Januari 21, 2023).