Wakala wa pembejeo, anayedaiwa kuchakachua mbolea na kuwauzia wakulima Mkoani Njombe hali iliyopelekea kuleta madhara makubwa ikiwemo kukauka kwa mazao ya baadhi ya Wakulima shambani, amefutiwa leseni.

Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Stephan Ngailo amesema uamuzi huo unakuja baada ya kukagua vidhibiti mbali mbali vilivyokamatwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa Mkoa wa Njombe.

Baadhi ya Wakulima Mkoani Njombe.

“Huyu amefanya udanganyifu,ubadhilifu na uhujumu uchumi hakuwa na nia njema na wakulima Kwa hiyo katika hatua ya kwanza tumeshamfutia leseni,huyu sio mfanyabiashara wa mbolea tena”Amesema Ngailo

Aidha, Ngailo pia ameagiza zoezi la kutafuta wafanyabiashara wabadhilifu lifanyike katika mikoa yote nchini, hasa ya nyanda za juu kisini ili kudhibiti vitendo hivyo huku akiagiza kuwafidiwa wananchi waliopata hasara ya kununua mbolea bandia.

Ajali ya Boti: Zaidi ya watu 150 wahofiwa kufa maji
Bashe awarudisha Darasani Wakulima