Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na mweka hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko wataendelea kusota rumande hadi Januari 3, 2019 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuahirisha kesi yao.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo akisaidia na wakili Salim Msemo wakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri wamedai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa.
Aidha, Mbowe na Matiko wako gereza la Segerea baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 23, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana ikiwemo kutoka nje ya nchi bila kibali.
Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ya jinai namba 112/2018 ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicenti Mashinji, Makatibu Naibu wakuu, Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara).
Wengine ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee, mbunge wa Bunda, Mchungaji Peter Msigwa, mbunge wa Tarime Vijijini na John Heche.
-
LIVE: Rais Magufuli akiwatunukia vyeo waliofanya vizuri zaidi mafunzo ya uofisa na ukaguzi
-
Video: Makonda anusurika mtego wa JPM ”Makonda bahati yako sana,”
Hata hivyo, Mbowe na viongozi wengine wanakabiliwa na mashtaka 13 ya uchochezi, uasi na kuhamasisha wafuasi wao kutenda makosa, hakuweza kufika mahakamani wakati kesi yao ilipotajwa.