Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa Watanzania wanapaswa kujua kuwa Tanzania ni kubwa kuliko chama.
Amesema kuwa jambo la msingi ni umoja na mshikamano ambao utawaweka Watanzania wote katika hali ya amani na undugu.
Aidha, ametaja vipaumbele vya chama hicho kwa mwaka 2018 kuwa ni kupigania kuundwa kwa Katiba Mpya na kutaka viongozi wa dini waachwe watoe maoni yao.
“Tutapigania katiba mpya, tume huru ya uchaguzi ili tupate uhuru wa kuongea zaidi na mara nyingi tumeishauri serikali kama hawaoni umuhimu wa kuwa na vyama vingi vya siasa ni bora wavifute,”amesema Mbowe
Hata hivyo, Mbowe amezungumzia hali ya kiafya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuwa imeimalika na atasafirishwa kutoka Nairobi nchini Kenya kwenda Ulaya kwaajili ya mazoezi zaidi.