Mke wa Mwanasiasa maarufu nchini na Mbunge wa Singida Viti Maalum (CHADEMA), Jesca Kishoa amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kusema kuwa watu wasiojulikana wamemfanya kiongozi huyo kuwa jasiri zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mbunge huyo amethibitisha kufika Hospitalini alikolazwa Mbunge Lissu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu huko mkoani Dodoma.

“Shauku yake ya kulitetea taifa hili imeongezeka mara 100000000000….. Aisee ni kama kuzima moto kwa petrol…Wasiojulikana wamemfanya awe jasiri zaidi.mungu ambariki sana,”ameandika Kishoa

 

CCM yazidi kunawili, wapinzani wengine 19 wajiunga
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 31, 2017